December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi yawahakikishia waandishi wa habari kulinda haki zao

Na Judith Ferdinand,Timesmajira online, Mwanza

Imeelezwa kuwa waandishi wa habari nchini wamekuwa walikutana na changamoto ya kiusalama wakati wa kutimiza majukumu yao hali inayochangia kuwanyima haki wananchi ya kupata habari.

Kwa kuitambua changamoto hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesisitiza kulinda haki ya waandishi wa habari katika kutafuta habari ili ziwefikie wananchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa wa tatu kushoto akiwa na Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko wa tatu kutoka kulia walio Kaa chini wakiwa na wanachama wa MPC katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari ambayo Mkoa wa Mwanza wameadhimisha Mei 16,2023 jijini Mwanza.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa,katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani,ambayo uadhimishwa kila ifikapo Mei 3, duniani huku kitaifa yalifanyika Zanzibar na kimkoa Klabau ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza(MPC) wameadhimisha Mei 16,2023,jijini hapa.

Ambapo ameeleza kuwa moja ya jukumu la jeshi hilo ni kulinda usalama wa wananchi na mali zao na suala la haki kwa watu wote wamelitanguluza mbele.

Hivyo wataendelea kulinda waandishi habari mkoani humo wakati wa kutimiza majukumu yao ili wananchi waweze kupata haki yao ya msingi ya kupata habari.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwenu waandishi wa habari katika kuhakikisha mnatafuta na kutoa habari kwenye maeneo ambayo tutakuna ya kikazi tunaahidi kuwalinda ili muwe salama na kuweza kuwafikishia wananchi habari,”ameeleza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo Mkoa wa Mwanza wameadhimisha Mei 16,2023

Sanjari na hayo Mutafungwa,amesisitiza MPC kuhimiza wamiliki wa vyombo vya habari kuwatafutia waandishi wao vitambulisho ili waweze kuwa salama katika utendaji kazi wao na kuwapa nafasi Polisi ya kuwatambua pale linapotokea tukio na pande zote mbili zikitekeleza majukumu yao.

Pia ameeleza kuwa ili waandishi waweze kufanya kazi vizuri lazima wazingatie weledi katika utendaji kazi wake na wawe na kitambulisho kinachomtambulisha chombo kwani matukio mengine yanakuwa ya dharura.

Hivyo wasipokuwa na kitambulisho inaleta ugumu katika utendaji kazi wa jeshi la Polisi na waandishi wa habari katika matukio yanayowakutanisha pamoja hususani ya dharura.

Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo Mkoa wa Mwanza wameadhimisha Mei 16,2023

“Kila mmoja afanye kazi kwa weledi ili wananchi wapate haki ya msingi ya kupata habari,sisi kama jeshi la Polisi kwa kutambua changamoto hiyo,tuna kauli mbinu yetu ambayo tunaisimamia isemayo,nidhamu,haki,weledi na uadilifu ndio msingi wetu,” ameeleza Mutafungwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko,amesema kwa Mkoa wa Mwanza umefanikiwa kuwa na mahusiano mazuri kati ya jeshi la polisi waandishi kwa kuitisha midahalo na kujadili kuhusiana na changamoto wanazopitia.

Soko ameeleza kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali katika ufanyaji wa kazi ikiwemo usalama wao huku akiwasisitiza waandishi wa hao kufuata sheria,kanuni na taratibu za taaluma hiyo wakati wakitekeleza majukumu yao.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo Mkoa wa Mwanza wameadhimisha Mei 16,2023