Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Ni zaidi ya siku 10 zimepita tangu Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kutoa taarifa ya watu watatu wa familia moja kupoteza maisha pamoja na uharibifu wa mali baada ya nyumba yao kuchomwa moto.
Ambapo chanzo cha kuchomwa moto nyumba hiyo ikielezwa ni kutokana na migogoro ya kimapenzi kati ya marehemu mwenye nyumba hiyo na hawara yake ambaye awali alikimbia baada ya kufanya tukio hilo kisa ni kumgombania mtoto ambaye ni miongoni mwa watu watatu waliopoteza maisha katika moto huo.
Hivyo kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye alikuwa amekimbilia kwa Mganga wa Jadi mkoani Geita.
Akizungumza namna walivyoweza kumkamata mtuhumiwa huyo kwa waandishi wa habari mkoani hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa ameeleza kuwa jeshi hilo limefanikiwa kumkamata Nestory John mwenye umri wa miaka 52 Mkulima na mkazi wa Buhongwa kwa tuhuma za kuhusika na kuchoma nyumba moto na kusababisha vifo vya watu watatu na uharibifu wa mali.
Ambapo ameeleza kuwa tukio la kuchoma nyumba lililofanywa na mtuhumiwa huyo lilitokea Desemba 7,2023 majira ya saa 6 na dakika 20 usiku eneo la Lwahnima Wilaya ya Nyamagana ambapo nyumba ya Eva Stephano(ambaye ni marehemu)ilichomwa moto na kusababisha vifo vya watu watatu wa familia moja na uharibifu wa mali.
“Baada ya tukio hilo kuripotiwa upelelezi na msako mkali uliifanyika na ilipofika Desemba 16,2023 majira ya 10 jioni huko Kata ya Nyang’wililela Tarafa ya Butundwe Mkoa wa Geita Askari Polisi wakifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa mafichoni kwa Mganga wa Jadi aitwaye Samson Mwinamila(35), mkazi wa Salagulwa mkoani humo akiwa anaoshwa dawa za kienyeji ili asikamatwe na polisi,”ameeleza Mutafungwa.
Pia ameeleza kuwa Mtuhumiwa huyo amekutwa na jeraha usoni lililotokana na moto huo wa mafuta baada ya kuripuka hivyo atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa