May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi Mbeya yapokea vitendea kazi kwa kamati ya usalama

Na Esther Macha, TimesmajiraOnline, Mbeya

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limepokea magari mawili na pikipiki mbili yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 31
kutoka kamati ya usalama barabarani ili kuweza kuongeza ufanisi wa ufanyaji kazi kwa Jeshi hilo hususani doria za barabara kuu,utoaji wa elimu na kuthibiti ukiukwaji wa sheria za usalama.

Akipokea magari mawili na pikipiki leo,Machi 4,2024 Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ,Benjamin Kuzaga ameishukuru Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya kwa msaada wa magari na Pikipiki hizo kwani zitasaidia katika kufanikisha kutekeleza majukumu kwa ufanisi na haraka.

“Msaada huu wa magari mawili na pikipiki mbili zitakuwa msaada mkubwa katika suala Zima la ulinzi na usalama pindi polisi wanapokuwa kwenye doria katika maeneo mbalimbali Jijini Mbeya katika suala la ulinzi na usalama barabarani kwa kuwa na ufanisi wa haraka kutokana na kuwa na vitendea kazi vya kutosha”amesema Kamanda Kuzaga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya ,Mhandisi Rajabu Ghuliku amesema kuwa kamati imeona vema kutoa msaada wa pikipiki na magari kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu katika Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Mbeya.

Aidha, Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Mrakibu wa Polisi, Hussein Gawile amesema kuwa, vitendea kazi hivyo vinakwenda kuongeza ufanisi na nguvu katika kuzuia na kudhibiti ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.