December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polepole ateuliwa kuwa Balozi nchini Malawi

Humphrey Hezron Polepole ameteuliwa na RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Zuhura Yunus

Taarifa hiyo inasema;

“Mheshimiwa Rais amewateua Bwana Humphrey Hezron Polepole kuwa Balozi wa Tanzania Nchi ya Jamhuri ya Malawi na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Ibara ya 67(2) (g) ikisomwa pamoja na Ibara ya 71(1)(a),”

Balozi Mteule Polepole wataapishwa tarehe 15 Machi, 2022 saa 04:00 asubuhi viwanja vya Ikulu, Chamwino, Dodoma.

Kabla ya uteuzi huo, Polepole alikuwa Mbunge wa Kuteuliwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo uteuzi wake ulifanyika Novemba 29,2020 na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.