November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Oparesheni Maalum za Jeshi la Polisi, SACP Mihayo Msikhela

Pikipiki, mali za wizi 825 zakamatwa Kanda ya Ziwa

Na Judith Ferdinand,Mwanza

MALI mbalimbali zikiwemo pikipiki  825 zimekamatwa katika operesheni  maalum ya kudhibiti vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi wa pikipiki katika mikoa ya Kanda ya Ziwa huku kesi 354 zikiwa zimefunguliwa.

Oparesheni hiyo ilianza rasmi Mei 4, mwaka huu kufuatia kazi iliyofanyika kwa wiki moja ya kukusanya taarifa za kiintelejensia  na za kiuhalifu ambayo.

Akizungumza Jijini Mwanza jana Mkuu wa Oparesheni Maalum za Jeshi la Polisi, SACP Mihayo Msikhela, amesema operesheni hiyo imefanyika kufuatia maelekezo ya awali ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirron kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kikao kilichofanyika Januari 22, mwaka huu mkoani Shinyanga.

Katika kikao hicho, IGP Sirro alielekeza kufanya operesheni maalumu kwa ajili ya kukabiliana na ongezeko la uhalifu wa wizi wa pikipiki katika mikoa hiyo hali ambayo inatishia amani katika maeneo hayo.

Operesheni hiyo imechukuwa takribani mwezi mmoja kuanzia Mei 4, mwaka huu na kukamilika Mei 29, mwaka huu ikihusisha mikoa nane ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Tarime Rorya, Mara na Kagera.

Alisema katika oparesheni hiyo Mkoa wa Mwanza walikamatwa watuhumiwa 12, injini za boti 106 katika visiwa vya Juma, Gembale na zilagula vilivyopo katika wilaya ya Sengerema,mkoa wa Tabora wamekamatwa watuhumiwa halisi watatu wa mauaji.