Na Bakari Lulela,Timesmajira
WAZIRI wa Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia na Utafiti kutoka Serikali ya Gambia, Prof. Pierre Gomez amesema amevutiwa na Sanaa ya mikono inayofanywa na chuo cha ufundi stadi VETA
ameyasema hayo leo juni 7,2025 katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere ( Sabasaba) wakati alipotembelea banda la veta ndipo alipofurahishwa na ubunifu wa vitendo zaidi kuliko nadharia
” Nilivyopita kwenye banda hili nimependa zaidi Sanaa za mikono zilizotengenezwa kwa ubunifu mkubwa hivyo nimefurahishwa sana” amesema Prof. Gomez
Aidha alipenda sana elimu ya Tanzani pamoja na ufundi stadi wa veta unaotolewa unapelekea watu kuendelea kuwa vizuri zaidi kwenye vitendo kuliko nadhalia
Pia ameongezea kwamba kwenye upande wa ubunifu ni mkubwa sana nimeona kwenye bidhaa zilizozalishwa na wanafunzi ni nzuri sana na zinavutia.
Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufudi stadi VETA CPA Antony Kasore amesema ugeni huu umekuja kujifunza mafunzo ya elimu na pia kujione maswala mbalimbali yanayofanyika kuhusiana na sayansi na techolojia pamoja na ubunifu nchini.
” Leo amekuja kwenye maonyesho ya 49 kimataifa ya biashara ( Sabasaba) ili kuangali Taasisi zote zilizopo chini ya wizara ya elimu jinsi zinazofanya kazi zake na wameweza kuona vitu mbalimbali vinavyofanywa na veta kuanzia kwenye utoaji wa mafunzo, kwenye ubunifu mpaka mwisho wa siku kuweza kuwafundisha watu ujasiliamali” amesema CPA Kasore
Ameongezea kwa kusema mafunzo yanayotolea ni muhimu sana mpaka yanapelekea mtu kujiajiri na kuanza kufanya shughuli za ujasiliamali na pia wameona wafunzo ya veta yalivyojikita kwa vitendo zaidi kuliko nadhalia.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako