November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PBWB kushiriki zoezi la kuzima Moto mlima Kilimanjaro

Na Martha Fatael,TimesMajira Online, Mweka

BODI ya maji bonde la Pangani (PBWB),ipo tayari kushiriki zoezi la kuzima Moto katika hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) ili kulinda vyanzo vya maji vilivyopo katika hifadhi hiyo.

Tayari PBWB, imetoa msaada wa kibinadamu wa vyakula na maji kwa vikosi vilivyopo mstari wa mbele katika kuuzima moto huo ambao Leo unafikia siku ya 10 tangu kuanza kwake.

Ofisa rasilimali watu wa PBWB Evagy Keiya, amesema hayo wakati akikabidhi msaada wa vyakula na maji kwa kaimu hifadhi ya Taifa ya mlima huo, Imani Kikoti ili kuvisaidia vikosi hivyo.

Amesema PBWB itashiriki kikamilifu katika jitihada za kuuzima Moto huo ili kuokoa vyanzo ambavyo vipo hatarini kukauka ama kuchafuka kutokana na athari za Moto huo.

Keiya amesema bonde ambalo linahusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na sehemu ya Manyara litahakikisha lina jukumu la kulinda rasilimali hizo.

Akipokea msaada huo Kaimu mhifadhi wa hifadhi ya Kilimanjaro [ KINAPA] Imani Kikoti ameishukuru bodi ya maji bonde la pangani kwa msaada huo.

Amesema bado PBWB wanaweza kupanda mlima huo ili kushiriki kuzima moto huo ama vinginevyo wanaweza kulipa vijana wafanyakazi hiyo kwa niaba yao.

Hata hivyo Mhifadhi Kikoti hakuwa tayari kuzungumzia Hali ya Moto katika mlima huo Kwa madai taarifa zitatolewa na viongozi wa ngazi za juu.