May 13, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PBPA yapongezwa kwa usimamizi wa upatikanaji wa Mafuta nchini

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA),Erasto Simon, amepokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Naibu Kamisha wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wahabi Matengo, kwa kutambua mchango na juhudi za taasisi hiyo katika kuhakikisha upatikanaji salama wa mafuta pamoja na uwepo wa bei shindani nchini.

Akikabidhi cheti hicho leo tarehe 13 Mei, 2026 jijini DaresSalaam, Matengo ameipongeza PBPA kwa kuendelea kusimamia kwa ufanisi mchakato wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja, hatua ambayo imeendelea kuisaidia Serikali kuongeza mapato kupitia ukusanyaji wa kodi na tozo mbalimbali.

Kwa upande wake,Erasto Simon amesema PBPA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unaendelea kuwa wa uhakika, salama na wenye kuwanufaisha wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla.

Amesema mafanikio hayo yanatokana na maboresho ya mifumo ya usimamizi wa mafuta, matumizi ya teknolojia za kisasa pamoja na ushirikiano mzuri kati ya Serikali na wadau wa sekta hiyo.