November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PASS Leasing inavyowainua wakulima

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

NAIBU Waziri wa Kilimo David Silinde amewaasa wadau wa masuala ya kilimo kuiga mfano wa PASS leasing wa kutoa matrekta  kwa wananchi 9 ambayo yanakwenda kurahisisha kilimo kwa wananchi hao na hivyo kuongeza tija.

Akizungumza katika banda la Agricom ambako zana hizo zilikabidhiwa kwa walengwa wakiwemo wanawake na vijana Silinde amesema ,kama Serikali itaendelea kuwaunga mkono .

“PASS Leasing  tunawashukuru kwa kazi mnayofainya ya kuwawezesha wananchi zana hizi za  kilimo ,na  hili ni jambo ambalo sisi kama serikali tutaendelea kuwasapot na inahitaji wadau kama ninyi kuhakikisha hii sekta ya kilimo tunaipush pamoja .amesema na kuongeza kuwa

“Na siku zote tumekuwa tulizungumza kwamba Sisi kama Wizara hatulimi,wanaolima ni wananchi na kilimo ni sayansi ambayo inahitaji ushirikiano wa pamoja ili kwenda mbele,kwa hiyo kwa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ana dhamira ya dhati kuhakikisha kwamba kilimo tunakibadilisha kwenye viwango vingine .

Silinde amesema, wizara imekusudia kwamba tuna’change’ tukitazame kilimo kwa mtazamo chanya kwa  kutumia Teknolojia za kisasa ambazo utarahisisha ulimaji lakini pia tunatransform kilimo chetu badala ya kutegemea mvua tiuqe na kilimo kinachotegemea maji kwa kujenga mabwawa ya umwagiliaji yatakayowezesha wananchi kulima kwa tija

Kwa upande wake Mkurugenzi Bodi ya PASS Leasing Rosebard Kurwijila amesema kampuni hiyo itawawezesha wakulima kupata zana zankilimo ili waweze kuzalisha kwa tija.

“Na tunapotoa vifaa hivi tunazingatia mnyororo wa thamani tangu kulima mpaka kuyaandaa mazao ,na mpaka sasa tumeshawawezeshabwakulima 1,000.”amesema Kurwijila

Baadhi ya wakulima walizokabidhiwa matrekta hayo  ameishukuru PASS Leasing kwa kuwapatia matrekta hayo ambayo wanakwenda kuwasaidia kuongeza tija kwao nanTaifa kwa ujumla.