December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Parachichi husaidia wakati wa msongo wa mawazo

Parachichi ina virutubisho kama ”nutrient dense fruit” vikiwa vimebeba kiwango kikubwa cha virutubisho vya protini, mafuta, vitamin, wanga na madini mbalimbali.

faida za kiafya za maparachichi ni pamoja na kumuweka  mtu katika hali nzuri (mood) kwani baadhi ya tafiti zimeeleza watu wenye msongo wa mawazo huwa na upungufu mkubwa wa madini ya Potasiamu na parachichi ni tunda lenye madini ya potasiamu.

Vitamini K inayopatikana kwenye parachichi husaidia unyonywaji wa madini ya kalsiamu ambayo hujenga mifupa na kuwa imara na kuondoa mifupa kulainika.

Parachichi moja lina kiasi cha asilimia 50 ya mahitaji ya vitamin K kwa siku.

Hutumika kutengeneza mafuta ya nywele na ya ngozi kutokana na kusheheni kwa vitamin E ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya.

Madini ya kopa yanayopatikana kwenye parachichi kwa zaidi ya asilimia 19 yana nafasi kubwa sana katika kuufanya ubongo ufanye kazi vyema.

Huongeza nguvu za mwili kutokana na kumiliki kiwango kikubwa cha virutubisho vya wanga, protini na mafuta,hupunguza lehemu mwilini ( Cholesterol).