November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Daktari akimpima paka ili kubaini kama ana maambukizi ya virusi vya Corona COVID-19

BREAKING:Paka wathibitika kuwa na virusi vya Corona

NEW YOK, Mamlaka jijini New York nchini Marekani zimethibitisha visa viwili vya aina yake kwa kubaini kuwa, paka wawili wameambukizwa virusi vya corona (COVID-19).

Hayo yamebainishwa na Shirika la Habari la CNN ambapo kupitia taarifa yake imebainisha kuwa, paka hao walibainika baada ya kuonekana kuwa na dalili za kupumua kwa shida.

“Hawa ni wanyama wa kwanza nchini Marekani kupimwa na kugundulikwa wameathirika,”ilieleza sehemu ya taarifa ya pamoja baina ya Idara ya Kilimo nchini Marekani na Kituo cha Magonjwa nchini humo.

Kwa mujibu wa taasisi hizo za umma, hakuna ushaidi wowote unaoonyesha kuwa wanyama hao wanaweza kueneza virusi nchini Marekani.

“Hakuna sababu ya kuchukua hatua dhidi ya wanyama rafiki, ambazo zinaweza kuathiri ustawi wake,”ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, paka hao walipimwa baada ya kuonyesha dalili zisizo za kawaida katika mfumo wa upumuaji, hivyo tayari wamechukuliwa na kupelezwa katika bustani ya wanyama ya New York zoo kwenda kuungana na simba na chui waliobainika kuwa na tatizo kama hilo siku za hivi karibuni.

Daktari wa wanyama mjini humo alichukua vipimo vya paka wa kwanza baada ya kuonyesha udhaifu katika mfumo wa upumuaji, ingawa katika nyumba ambayo alikuwa anafugwa hakuna mtu ambaye alithibitika kuwa na virusi hivyo.

“Inawezekana paka aliambukizwa na mtu nje ya nyumba, kwa sababu ndani ya nyumba hakuna aliyebainika kuwa na dalili za virusi ambaye angeweza kumuambukiza paka,”alieleza Daktari huyo.

Kwa mujibu wa CNN, paka wa pili katika eneo tofauti la jiji la New York, pia alipimwa baada ya kuonekana na viashiria vya dalili zisizoridhisha katika mfumo wa upumuaji.

Awali kwa mujibu wa CNN, mmiliki wa paka huyo alipimwa na kugundulika ameambukizwa virusi vya corona, kabla ya paka kuumwa, lakini paka mwingine ndani ya nyumba hakuonyesha dalili yoyote ya ugonjwa.

Habari kamili soma Gazeti la Majira…