Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, ameahidi kuhakikisha uchaguzi wa 29 Oktoba 2030 unakuwa huru, haki na wenye uwazi, sambamba na kupambana na ufisadi mara baada ya kuingia madarakani.
Aliyaeleza hayo huko viwanja vya kibandamaiti Mkoa wa Mjini Unguja katika siku ya mwisho kufunga kampeni
Othman amesema yeyote atakayebainika kufanya ubadhirifu wa ardhi au fedha za umma atachukuliwa hatua kali za kisheria bila kuonewa huruma.

Mtu yeyote ambaye amenyang’anywa ardhi yake, serikali yangu itamrejeshea ardhi hiyo au kumpa fidia inayolingana na thamani ya mali yake,” amesema Othman.
Aidha, ameahidi kwamba kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa serikali kitakuwa shilingi milioni moja, hatua ambayo inalenga kuboresha maslahi na maisha ya watumishi wa umma.

Othman pia amesema vikosi vya SMZ vitarejeshwa katika majukumu yao halisi, na havitatumika tena kwa kazi ambazo hazihusiani na dhamira ya kuwalinda wananchi.
Katika upande wa elimu, amesema walimu watapewa heshima zao na kuishi maisha bora zaidi kutokana na kuboreshwa kwa mishahara na mazingira ya kazi.

Kwa wazee, Othman ameahidi pensheni ya kila mwezi ya shilingi 120,000, pamoja na bima ya afya bure kwa wazee wote ili kuhakikisha wanapata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

Akigusia sekta ya kilimo, Othman amesema serikali yake itaimarisha kilimo cha karafuu na mazao mengine ya biashara ili kuongeza kipato cha wakulima na kukuza uchumi wa Zanzibar.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako