January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Januari 06, 2025 amekabidhiwa Jezi ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes).

Mheshimiwa Othman ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa ACT- Wazalendo amekabidhiwa Jezi hiyo, kutoka kwa Naibu Waziri Kivuli wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, wa Chama hicho, Ndugu Humoud Ahmed Said, hapo Ofisini kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Migombani Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja.