Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, amejumuika na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, hapo Msikiti wa Mfereji wa Wima, Ng’ambu, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja.
Ibada hiyo iliyowajumuisha Viongozi mbali mbali wa Dini, Siasa na Jamii, akiwemo Katibu wa ACT- Wazalendo Mkoa wa Mjini kichama, Bw. Mahmoud Ali Mahinda, iliyofanyika Oktoba 28, 2022, imehusisha pia Dua Maalum ya Kuwaombea Viongozi, Masheikh, Wazee, na Wananchi Wema walioko hai na pia ambao wameshatangulia Mbele ya Haki kwa ujumla.
Dua hiyo imeongozwa na Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume.
Kabla ya Dua hiyo, Khatiib Sheikh Abdulkarim Said Abdullah, kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, ametoa Khutba Mbili za Ijumaa zilizoweka msisitizo kwa Waumini, juu ya Umoja, Mshikamano na Utiifu kwa Viongozi Wema, kama ilivyosisitizwa katika Misingi ya Dini ya Kiislamu.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini