Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Januari 12, 2024, amejumuika na Viongozi wa Serikali, Marais kutoka Nchi mbali mbali, Wanasiasa, Viongozi Wastaafu, Mabalozi na Wanadiplomasia, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wananchi wa Mikoa Mitano ya Unguja na Pemba na Tanzania Bara, katika Hafla ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hafla hiyo ambayo imefanyika katika Uwanja wa New Amani Complex, Mkoa wa Mjini- Magharibi Unguja, imeongozwa na Mgeni Rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na kuhudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan.
Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Othman ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua