January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Othman ashiriki kikao kamati kuu ACT-Wazalendo

Makamu Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Zanzibar ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, leo Jumapili Machi 3, 2024, amejumuika na viongozi wengine wakuu wa chama hicho katika Kikao cha Kamati Kuu.

Kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Juma Duni Haji, ndani ya Jengo la Maalim Seif, Makao Makuu ya ACT- Wazalendo Magomeni Mikumi, jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Taifa, Juma Duni Haji, kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Kiongozi Mkuu wa chama hicho Zitto Zuberi Kabwe.

Viongozi wengine ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Tanzania Bara, Doroth Semu; na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu Ado.