Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online
WAKALA wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA),imetoa wito kwa waajiri nchini kuhakikisha wanafuata sheria za afya sehemu ya kazi ili ufanisi uongezeke zaidi.
Akizungumza nkatika viwanja vya maonesho ya 45 ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Ofisa Habari Mwandamizi kutoka OSHA, Paul Gyuna amesema afya sehemu ya kazi ni muhimu kutiliwa mkazo wakati wote kwa kutokana na kuleta tija ya kukuza uchumi .
Gyuna amesema katika chunguzi zao wanazozifanya sehemu mbalimbali wanazopitia wanaona changamoto ya afya sehemu ya kazi haipo sana tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Amesema kutokuwepo kwa changamoto hiyo imetokana na elimu inayotolewa mara kwa mara na maafisa wa osha wanapotembelea sehemu za kazi.
“Kuna umuhimu mkubwa wa kufuata sheria za afya sehemu ya kazi ili utendaji wa kazi uende vizuri kwa ajili ya kukuza uchumi”amesema Gyuna.
Gyuna amesema, bado kuna uelewa mdogo wa baadhi ya wafanya kazi wasiojua haki zao hadi hivi sasa ikiwemo kustahili kuwepo katika mazingira safi na salama sehemu zao za kazi.
“Hivi sasa tumehakikisha sehemu yeyote ya kazi ni lazima kuwepo na mazingara mazuri kwa ajili ya watu wenye ulemavu hususani maliwatoni”amesema.
Vilevile alisema OSHA inahakikisha kila mfanyakazi ni lazima kupima afya wakati wa kuajiriwa,anapofanya kazi na anapostaafu au kuacha .
Amesema hiyo itamsaidia muajiri wake kuweza kumpanga sehemu inayostahili zaidi kutokana na matokeo ya afya yake.
“ Mwajiri anaweza kumpa mfanyakazi kazi ngumu ambayo afya yake haistahili lakini akijua afya yake ataweza kumpa kazi anayoendana naye.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi