*Watatu Mwanza washinda zawadi kupitia kampeni ya Gesi Yente
*Lengo ni kufikia asilimia 80 ya watanzania wanaotumia nishati safi
*Taasisi binafsi,umma zatakiwa kuondokana na matumizi ya mkaa
Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Wito umetolewa kwa taasisi binafsi na za Serikali ambazo zina watu zaidi ya 100,kuondoka na matumizi ya kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati safi ikiwemo gesi.
Huku kampuni ya gesi ya Oryx kuendelea kuunga mkono Serikali kwa kuendelea kutoa zawadi kwa wateja wanao tumia gesi ili kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi.
Hayo yameelezwa Septemba 2,2025 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana Thomas Salala wakati wa zoezi la kuwakabidhi zawadi washindi wa kampeni ya Gesi Yente inayoendeshwa na kampuni ya Oryx Enegies,kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Ambapo katika zoezi hilo jumla ya washindi watatu kutoka Mkoa wa Mwanza wamepatiwa zawadi ikiwemo mmoja aliyepata pikipiki huku wawili wakizawadiwa baiskeli.
“Hiki mnachokifanya cha kutoa zawadi kwa wateja wenu ni kizuri,kuna watu wanavutika akienda mtaani akasema pikipiki hii nimepewa na watu wa Oryx inaongeza chachu.Na mmesema kampeni hii siyo kamali lakini ni kurudisha kwa wananchi,”amesema Salala.
Salala amesema,kupitia kampeni hiyo na hamasa hiyo baada ya miaka fulani watashuhudia matumizi makubwa ya nishati safi yanaongezeka kwa wananchi.
“Pia naamini mtatengeneza fedha,uchumi wenu wenyewe, mtalipa kodi serikalini na sisi tutashangilia, kwa sababu tunahitaji kodi ili barabara zijengwe,maji yapatikane na shughuli nyingine za kiuchumi zifanyike,”amesema Salala.
Hivyo amesisitiza mawakala wa nishati ya gesi ikiwemo ya Oryx,kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya faida za matumizi ya nishati safi ikiwemo gesi huku Serikali ngazi ya Wilaya zipo juhudi ambazo inazifanya ikiwemo kusimamia taasisi binafsi na za imma zenye watu wengi,ili watoke kwenye matumizi ya kuni watumie nishati safi ikiwemo gesi.
“Uelekeo wa nchi ifikapo 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi.Kama Wilaya tunalipokea jambo hili kama ilivyoelekezwa na Serikali,”amesema Salala na kuongeza:
“Moja ya maeneo ambayo tumeanza kutumia nishati ya gesi ni shule yetu ya sekondari ya Nsumba,ina wanafuzi zaidi ya 1000,kwa sasa hakuna matumizi ya mkaa wala kuni.Pia kwenye gereza letu la Butimba ambalo tuna watu wengi wameanza kuachana na matumizi ya kuni,hii ni moja ya jitihada ambazo tumezifanya kuhakikisha kwamba tunakuwa sehemu ya kuitika katika mpango huo,”.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko Oryx Gas Tanzania,Shaban Fundi,amesema uelewa wa wananchi wa kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi umeongeza na mwitikio umekuwa mkubwa mpaka maeneo ya vijijini.
Fundi amesema,licha ya mafanikio hayo bado hamasa inatakiwa ili kufanya wananchi waendelee kutumia nishati hiyo,ambapo wao kama Oryx wanafanya hamasa hizo mpaka vijijini ili hata wale waliopata mtungi wa gesi kupitia programu mbalimbali waweze kuendelea kutumia wakati wote wasiiache mtungi ndani.
Ambapo amesema,ndio maana wameamua kuja na kampeni hiyo ya Gesi Yente ambayo imelenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuokoa taifa kutokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
“Kupitia kampeni hii ilioanza Agosti 13,2025,wateja wetu wa gesi ya oryx wanapata zawadi.Mpaka sawa wateja wasiopungua 350 wamefanikiwa kupata zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki,baiskeli na sufuria za kupikia kwenye jiko la gesi,”amesema Fundi.

Naye mshindi wa pikipiki kupitia kampeni hiyo,Maximilian Nyamoge amesema alihamasika kutumia nishati ya gesi kwa sababu haina usumbufu wakati wa kuwasha kama kuni na mkaa na kwamba inawahisha mapishi.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako