Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania kwa kushirikiana na Tanzania Communities Rise Foundation(TCRF) wamezindua jiko linatumia mfumo wa nishati safi katika shule ya sekondari Yusuf Makamba iliyopo mkoani Dar- es-Salaam, lengo likiwa ni kuondoa matumizi ya mkaa katika shule hiyo yenye wanafunzi 1391.
Akizungumza Septemba 19,2025 katika hafla ya uzinduzi wa jiko hilo,Mkuu wa Masoko na Mauzo kutoka Oryx Gas,Shaban Fundi,amesema kampuni yao kwa kushirikiana na TCRF wameweka jiko la nishati safi ya kupikia kwa sababu ni moja ya jitihada zao za kuona Watanzania wanatumia nishati hiyo.

Fundi amesema, Serikali kupitia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imekuwa na ajenda kuu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo katika taasisi zenye watu zaidi ya 100.Hivyo kufunga mfumo huo katika shule hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika eneo la nishati safi.
“Kampuni ya Oryx Gas kama wadau wa nishati safi tumeona tuoneshe mfano na kuthibitisha uwezo wetu mkubwa katika kufanya miradi ya kufunga mifumo ya nishati safi ya kupikia,”amesema Fundi.
Fundi amesema jiko la nishati safi ya Oryx katika shule hiyo inakwenda kunufaisha wanafunzi 1391 ambao kila siku wanapokuwa shule wanapikiwa chakula
“Matumizi ya kuni na mkaa waliyokuwa wanatumia kuandaa chakula kıla siku yalikuwa makubwa pia yalikuwa na changamoto za kiafya.Hapa kuna wanafunzi ,walimu na wapishi hivyo walikuwa wanapata adha ya moshi,”amesema.
Pia amesema,walianza kuufunga mfumo kama huo katika shule ya sekondari Kiluvya na wameanza kutoa udhamini kwa shule hizo mbili ambazo zina wanafunzi wengi.
Kwa upande wake Mkurugenzi na Muanzilishi wa Taasisi ya Tanzania Communities Rise Foundation,Sarah Ngoma,amesema wamechagua kushirikiana na Oryx kwa sababu ndio kampuni kinara katika soko la gesi ya LPG na wanajukulana nchi kote katika biashara ya mitungi ya gesi na majiko yake.
Pia amesema wamekuwa wakishirikiana na Oryx Gas katika matukio mengi hasa yanayohusu nishati safi sambamba na kuwezesha mama lishe kutumia nishati hiyo badala ya kutumia nishati nyingine ambazo sio rafiki wa mazingira.

“
“Sisi kama taasisi hatufanyi tu shughuli hizi hapa Dar-es-Salaam lakini tuna ratiba za nishati safi mikoani ikiwemo Mkoa wa Lindi maeneo ya vijijini hivyo kampuni ambayo inaweza kuwafikia tunaowalenga tunaona mwenye uwezo huo ni Oryx.”
Pia amesema wanayo kanzi data shule zaidi ya 10 ambazo walizifanyia utafiti lakini wameanza na shule ya Sekondari Yusuf Makamba iliyopo mkoani Dar es Salaam kwasababu iko katikati ya mji na inatumia mkaa.
“Hivyo unaweza kuona wanaothirika sio tu walioko ndani ya shule bali hata wale walioko nje ya shule hii,”amesema.
Amesema kitendo cha kuona shule hiyo bado inatumia nishati chafu ndipo waliona kuwa iko haja ya kujenga mfumo wa jiko ambao utatumia nishati safi ya kupikia hivyo kwa kushirikiana na Oryx Gas wamefunga mfumo huo.
Ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau ,mashirika na taasisi kusaidia zaidi kwenye taasisi mbalimbali hususani zenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili waweze kutumia Nishati safi ya gasi.

NayeMkuu wa Shule ya Sekondari Yusuf Makamba iliyopo jijini Dar es Salaam,Kanne Kibangali,amesema kufungwa kwa jiko la oryx katika shule hiyo kwao ni neemakwani inakwenda kurahisisha utendaji kazi,kwa sababu wanafunzi ni wengi na wanapoandaa chakula wamekuwa wakitumia muda mwingi.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako