Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
KatikakuhakikishaajalizinakomeshwakatikamkoawaArushaJeshilaPolisi mkoawaArusha kupitia kikosi cha usalama barabarani pamoja na wakuu wa Polisi wilaya (OCD’s) mkoani hapa wameendelea kuimarisha operesheni ya kuwakamata na kuwachukulia hatua madereva wote wanaokiuka sheria na taratibu za usalama barabarani.
ACP MAasejo amesema Katika operesheni hiyo madereva watakaoendesha vyombo vyamoto kwakutozingatia sheria hususani mwendo kasi, wakiwa wamelewa ama kujaribu kupita magari mengine bila kuchukua tahadhari (overtaking), hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kuwakamata
na kuwafikisha mahakamani kwani imebainika madereva wengi wanaamini wakivunja sheria watalipa faini.
Amesema kuwa ameshatoa maagizo kwa Mkuu wa Polisi Kikosi cha usalama barabaran pamoja na wakuu wa Polisi wilaya zote kuhakikisha wote wanakuwa barabarani katika kusimamia operesheni hizo.
Sambamba na hilo Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusiana na madereva wote wanaokiuka sheria na taratibu za usalama barabarani ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao
Katika tukio jingine kamanda masejo amesema Tarehe 01. 04. 2022 muda wa saa 04:00 asubuhi huko maene oya Osunyai katika Halmashauri ya Jiji la Arusha askari wakiwa doria walifanikiwa kumkamata AbdiHamis (27) mfanyabiashara, mkazi wa Ngarenaro na Ally Said (25) dereva na mkazi wa Olasiti Jijini Arusha wakiwa wanasafirisha madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni Heroin gramu
70.77 kwa kutumia gari Na.T949DQA aina ya Mercedes Benz ikiwa na tela Na.T. 253CXR.
ACP Masejo amesema Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu kwa muda mrefu na walikuwa wakifuatiliwa.
Aidha bado tunaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao pamoja na gari hilo na pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha ameendelea kusema Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kipindi cha mwezi March 2022 lilifanya operesheni mbalimbali ambazo zilifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 87 wanaojihusisha na makosa mbalimbali hususani madawa ya kulevya.
Waliokamatwa ni watuhumiwa 22 wakiwa na bhangi misokoto 678, watuhumiwa 18 wakiwa na mirungi bunda 22, watuhumiwa 06 wakiwa na kete 7 za madawa ya kulevya aina ya Heroin pamoja na watuhumiwa 41 wakiwa na pombe ya moshi lita 24.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa watu wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na vitendo vya kiharifu na waharifu ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba