Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeweka kambi katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma ili kutoa huduma mbalimbali zinazohusu masuala ya kisheria kwa wananchi wanaotemebelea banda la Ofisi hiyo.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo Wakili wa Serikali Mkuu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jackson Nghoboko,amesema kuwa Ofisi hiyo imeendelea kutoa elimu na ushauri wa Kisheria pamoja na kutatua migogoro na malalamiko yanayowakabili wananchi.
“Tunaendelea kutoa elimu na ushauri wa kisheria kwa wananachi wanaokuja hapa, pia migogoro inayohusu masuala ya Ardhi, ndoa na masuala ya ya matunzo ya watoto tumekuwa tukiipokea na kuishughulikia.” amesema “. Nghobolo
Aidha,Nghoboko ametoa wito kwa wananchi wa Jiji la Dodoma kuendelea kujitokeza kwa wingi katika banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za Kisheria zinazowakabili wananchi.
Alitoa rai kwa wananchi wa Dodoma waende kwenye banda hilo lililoko katika maadhimisho ya Utumishi wa Umma hapa Chinangali wahudumiwe huduma zote wanazitoa hapo ni bure.
Kwa upande wake mmoja ya wananchi waliotembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Magreth Kapele amefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mawakili wa Serikali katika banda hilo, ikiwemo ushauri wa kisheria unaotolewa.
“Nimefika kwenye banda hili la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali nimehudumiwa vizuri, maswali mengi ambayo yalikuwa yananitatiza nimejibiwa kwa ufasaha kwakweli nimejifunza mambo mengi.”amesema Magreth
Naye, Eduard Sunday, ameishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutoa huduma bora kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kulipia huduma za kisheria, pia ameipongeza Ofisi hiyo kwa kutoa huduma kwa haraka na kwa urahisi .
“Naishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutupatia huduma kisheria bure na kwa haraka, nimefika hapa nimehudumiwa vizuri na Mawakili nawapongeza sana.” amesema Sunday
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 Juni 2025 na yanaendelea hadi tarehe 23 Juni, 2025, ambapo Ofisi hiyo inaendelea kutoa huduma za Ushauri wa Kisheria, Elimu ya Sheria, Utatuzi wa Migogoro na Kushughulikia Malalamiko ya Wananchi.



More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako