Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa ushauri wa masuala ya kisheria bure kwa wananchi Ili kuwapa Elimu kuhusu masuala hayo.
Aidha,ofisi hiyo imewataka wananchi kutembelea Banda lao katika viwanja vya Nyerere ili waweze kupata Elimu hiyo.
Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali Kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Theresia Sanga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la ofisi hiyo kwenye maonesho ya wiki ya Sheria nchini yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere jijini Dodoma.
Alisema kuwa ushauri wa kisheria wananchi wataupata kwa asilimia 100 bila malipo ya aina yoyote pindi watakapotembelea banda hilo.
“Katika maadhimisho haya,ushauri wa kisheria tunatoa bure katika Banda letu tofauti na nyakati zingine au kwenda kwa mawakili wankujitegemea ambapo huduma hiyo inalipiwa,
“Kwa hiyo kitu ambacho wananchi hawawezi kukipata kutoka Ofisi yetu ni ule uwakilishi wa wakili mahakamani ,hivyo baada ya kupata ushauri akitaka uwakilishi ataenda kutafuta kwa wanasheria ambao ni wale mawakili wa kujitegemea.”alisema Sanga
Kwa mujibu wa Wakili Sanga, kwa ujumla ofisi hiyo inashugulika na utoaji ushauri wa Taasisi za Serikali, Halmashauri, wizara zote pamoja na mashirika yote ya Umma.
“Tupo katika maadhimisho ya wiki ya Sheria ikiwa na kaulimbiu ‘isemayo ni Tanzania ya mwaka 2050 nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ‘ ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni moja ya taasisi ambazo zinasimamia haki madai,” alisema.
Alisema kuwa tangu maadhimisho hayo kuanza wamepata mafanikio ya kupunguza migogoro, malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali.
“Endapo ikitokea mwananchi alikuwa na malalamiko dhidi ya serikali ofisi yetu kwa kuwa ndio mshauri Mkuu wa Serikali tunahakikisha suala hilo tunalimaliza kwa njia ya amani na majadiliano pasipo kufikishana mahakamani ili kuepusha hasara pamoja na kuwa acha wananchi wakiwa na amani, imani na serikali yao,” alieleza Sanga.
Aidha aliwasisitiza wananchi kwenda kutembelea banda hilo kwa kuwa ni nafasi ya kipekee ambayo mtu anaweza kuipata bila malipo na jambo lake likatatuliwa papo kwa papo na kuepuka kuzunguka kumtafuta wakili.
More Stories
Katibu Mkuu Nishati aipongeza Sweden kufadhili miradi ya umeme nchini
RAS Seneda akabidhi msaada wa Mablanketi kwa wazee na yatima
Balozi Nchimbi:Mapambano ya uhuru wa kiuchumi Kusini mwa Afrika yanaendelea