September 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ofisi Ardhi yanzisha mkakati kufuatilia hati za ardhi

Na Munir Shemweta,TimesMajira Online. Babati

OFISI ya Ardhi Mkoa wa Manyara, imeanza mkakati maalumu wa kwenda Ofisi za Ardhi katika halmashauri za wilaya, kuzifuatilia hati za ardhi ambazo haziwasilishwi kwenye ofisi hiyo kwa wakati, ili kujua changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi.

Mkakati huo unakuja Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Manyara, kuzishambulia kwa nguvu hati zilizopelekwa katika ofisi hiyo zikiwemo zilizokuwa na marekebisho na kuzimaliza zikitokea iliyokuwa Ofisi ya Ardhi Kanda ya Kaskazini (Moshi) iliyojumuisha Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Hayo yamesemwa leo na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Manyara, Leonard Msafiri wakati akielezea utendaji kazi wa ofisi yake tangu na kuzinduliwa rasmi Julai mwaka huu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

“Sisi kama Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Manyara, tumeamua kuja na mkakati maalumu wa kwenda katika wilaya kuzitafuta hati zilizopo kule kwa nini haziji na ‘why’ haziendi kwa kasi kubwa,” amesema Msafiri.

Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi, tayari ofisi yake imeanza kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto za sekta ya ardhi katika halmashauri za mkoa huo na kutolea mfano Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika suala la uandaaji.