January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nyashinski kutumbuiza “SERENGETI LITE OKTOBAFEST” Dar

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

MSANII maarufu nchini Kenya Nyamari Ongegu “Nyashinski” amewasili Tanzania kwa ajili ya tukio kubwa lililoandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti “OKTOBA FEST” ambalo litafanyika Oktoba 21, 2023 Coco Beach Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mara baada ya kuwasili leo jijini Dar es Salaam Msanii Nyashinski amesema kuwa kupata nafasi ya kutumbwiza jukwaa moja na wasanii mbalimbali wakubwa nchini Tanzania kama Alikiba ni jambo zuri ambalo litasaidia kufungua milango ya kufanya kazi na wasanii wa hapa kwa sababu ni matamanio makubwa kwa kila wanamuziki wa Kenya.

Tamasha hilo la “SERENGETI LITE OKTOBA FEST” litajumuisha wasanii lukuki kutoka hapa Nchini Tanzania wakiongozwa na Alikiba, billinas, Chino kidd, Gnako na Msanii kutoka nchini Uganda Jose Chameleon.