Na Jackline Martin, TimesMajira Online
KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha, Premer Bet imemtangaza mshindi kuwa, Nurdin Abdalah amejishindia Tsh 122,730,200/-, baada ya kubashiri matokeo sahihi ya mechi sita ya michezo ya mpira wa miguu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa kukabidhi fedha kwa mshindi huyo, Meneja Masoko wa Premier Bet, Eric Kirita alisema michezo ya kubahatisha siyo michezo ya ajira bali waichukulie kama sehemu ya burudani.
“Tunayo furaha kubwa kutangaza ushindi mkubwa Nurdin Abdalah, ambaye ameshinda Tsh. 122,730,200/-, kupitia michezo ya kubahatisha na burudani ya Premier Bet. Hii ni habari njema na tunayo furaha kuwa sehemu ya safari hii ya kushangaza,” alisema Kirita.
Kirita alisema, wao kama Premer Bet watampa ushauri wa kifedha mshindi huyo ili aweze kuendeleza biashara yake na kufikia malengo.
“Tunampongeza Nurdin Abdalah kwa ushindi wake mkubwa na tunamtakia mafanikio zaidi katika siku zijazo. Premier Bet inaendelea kujitahidi kutoa uzoefu wa kipekee wa kubahatisha na burudani, na tutampa ushauri wa matumizi ya fedha zake kutokana na biashara anayoifanya,” alisema.
Mwakilishi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Chiku salehe alimtaka mshindi huyo kutumia fedha hizo vizuri katika kufanya maendeleo.
“Leo tupo hapa katika kusimamia ushindi wa Nuridin aliyeshinda Milioni 122 ambapo tumefika hapa ili kuthibitisha kuwa ushindi huo ni wa halali na ni sahihi na pia tunathibitisha kuwa pesa zake atazipata kupitia Account yake. Tunamshauri Nurdin atumie pesa yake vizuri katika kufanya maendeleo ili kuendeleza nchi yetu,” alisema.
Hata hivyo alisema, mchezo huo wa kubahatisha unachezwa na watu kuanzia miaka 18 kwenda juu na siyo chini ya miaka 18.
Kwa upande wake mshindi wa mchezo huo, Nurdin Abdalah aliushukuru uongozi wa premier Bet kwa ushindi kwani kipindi Cha nyuma alikua akicheza na kushinda kiasi kidogo ambapo kwa sasa amefikia hatua ya kupata ushindi mkubwa wa shilingi milioni 122.
“Baada ya kupata ushindi Premier Bet walinipigia kupitia wakala na hawakuzungusha, hivyo nashukuru kwa kunipa ushindi huu.
“Mimi ni mfanyabiashara katika upande wa vifaa avya umeme, hivyo fedha hizi nitaziongezea katika biashara yangu nnayoifanya, kupitia ushindi huu unanipa mimi nguvu hata kwenye biashara zangu na hivyo nitafikia ndoto zangu”
Alisema, fedha zake atazitumia katika biashara yake ya vifaa vya umeme ambayo amekua akiifanya kila siku.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania