December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NSSF ilivyoshiriki katika maonesho ya Utalii Karibu Kusini Mkoani Iringa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulishiriki katika Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Kihesa Kilolo mkoani Iringa.

Maonesho hayo yalifungwa na Mgeni Rasmi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud.

NSSF ilitumia maonesho haya kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi,kuandikisha wanachama, kusikiliza na kutatua kero za wanachama.