Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
MAKUMBUSHO ya Taifa la Tanzania (NMT) imeendesha mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa watumishi wake, kwa lengo la kuimarisha usalama wa watu, mali na miundombinu ya taasisi.
Mafunzo hayo yamefanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Posta, jijini Dar es Salaam, na kufunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa NMT, Dkt. Noel Lwoga, akifuatana na Mkurugenzi wa Huduma na Shirika, Zakkarriya Kyera, pamoja na Mkuu wa Utawala na Rasilimaliwatu,Renalda Lyimo.

Wawezeshaji kutoka Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, wakiongozwa na A/INSP Mohamed Selungwi, FC Eliamani Mwanga na FC Jofrey Sindika, waliwapatia watumishi elimu kuhusu visababishi vya moto, aina za moto, vifaa vya kudhibiti moto na taratibu za kuchukua hatua wakati wa dharura.
Kupitia mafunzo hayo, NMT inalenga kujenga utamaduni wa kuzingatia usalama kazini na kulinda watumishi, wageni, mali na miundombinu ya taasisi.




More Stories
SGA yaimarisha utoaji huduma bora kwa wateja
Tanzania yajipanga kuvutia uwekezaji Mkubwa wa Nishati Duniani
PREMIER BET yaunga mkono uhifadhi wa Mazingira