Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya elimu katika shule tano za halmashauri ya wilaya ya Kilosa na Mvomero vikiwa na thamani ya Sh. Mil 35 milioni ikiwa sehemu ya kupunguza changamoto za elimu mkoani Morogoro.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mabati, mbao, misumari na madawati kwa shule za sekondari Murrad Sadiq Sekondari, Mziha Sekondari huku kwa shule za msingi ni Madizini, Mlali, Matongolo na Mkwatani.
Wakizungumza wakati wa hafla iliyofanyika katika shule hizo kwa nyakati tofauti, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Matongolo wilaya ya Kilosa, Sifa Jonas alisema shule hiyo imepokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya Sh.Mil 5 ambayo yatasaidia tatizo la wanafunzi kukaa chini wakati wa masomo yao ya kila siku.
Sifa alisema shule ya msingi Matongolo ina jumla ya wanafunzi 2379 wavulana wakiwa 1155 na wasichana 1224 huku kukiwa na madawati 236 huku kukiwa kukihitajika madawati 557.
Shule ya Sekondari Murrad Sadiq Mvomero na shule ya Sekondari Mziha zimepokea vifaa vya kuezekea majengo ya vyumba vya madarasa kila mmoja vyenye thamani ya Sh. Mil 5 ili kukabiliana na wimbi la wanafunzi wataojiunga na kidato cha kwanza Januari mwaka 2023.
Mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Madizini wilaya ya Mvomero, Najma Ally amesema shule yao inakabiliwa na changamoto ya wanafunzi wengi kukaa chini na msaada huo wa madawati 50 vitasaidia kupunguza changamoto ya wao kukaa chini.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema benki hiyo kwa mwaka huu imetenga kiasi cha zaidi ya sh. Bilioni 2 kwa ajili ya kusaidiana na serikali kutatua changamoto katika sekta ya elimu, Afya na yanapotokea majanga.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi