Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya tiba mbalimbali kwa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba ikiwa ni utekelezaji wa azma yake ya kusaidia utoaji wa huduma bora za afya.Mchango wa benki hiyo unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashuka 200, mapazia ya wodini wodini 10, viti vya magurudumu 5 kwaajili ya kusaidia wagonjwa na mashine tatu za kupimia presha.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba, Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar, Naima Said Shaame alisema mchango wa benki hiyo unatokana na dhamira yake ya kusaidia ujenzi wa Taifa lenye afya bora.
Aidha, aliongezea kuwa benki yake inatoa kipaumbele kwa sekta ya afya na kusistitza kuwa sekta hiyo ni moja ya nguzo kuu za Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii na inawajibika kwa asilimia moja ya faida baada ya kodi (PAT) kugharamia mipango mbalimbali ya kijamii katika maeneo yake ya kipaumbele ikiwemo afya, elimu na dharura.
Na mpaka sasa, imechangia kwa kiasi kikubwa katika hospitali mbalimbali nchini na kuongeza kuwa michango ya benki hiyo inaleta mabadiliko makubwa katika kuinua viwango vya utoaji wa huduma za afya nchini kote.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Mwinyi akiwa ni mgeni rasmi wa uzinduzi huo, alipokea vitu hivyo kwa niaba ya Hospitali ya Wilaya na kuishukuru benki hiyo kwa ukarimu wake na kuongeza kuwa uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni ni njia bora ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu.
Lakini pia, aliwataka watoa huduma wa Hospitali hiyo ya Wilaya kutoa huduma bora kwa wateja kwani ni sehemu muhimu katika utoaji wa huduma za afya huku Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui alisisitiza dhamira ya Wizara yake ya kutunza miundombinu katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni ili kutoa huduma bora za afya kwa Wazanzibari wote bila ya ubaguzi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba