November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yaipa kipaumbele Uwezekaji kwa watu wake

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kupitia programu ya Mwanamke Kiongozi (Female Future Programme) inayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) – yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuwaongezea ujuzi wanawake katika uongozi ili waweze kumudu nafasi za juu za uongozi, wafanyakazi 7 wa benki Ya NMB wamehitimu mafunzo hayo katika Mkutano wa 5 wa Mwaka wa Uongozi ulioambatana na Mahafali ya Programu hii ya mafunzo jana jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika mkutano huu – Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), aliyeambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb).

Katika mkutano na mahafali hayo, Afisa Mkuu wetu wa Huduma Shirikishi wa NMB – Nenyuata Mejooli alisema “Benki ya NMB imekuwa ikitoa udhamini kwa wafanyakazi wake kushiriki mafunzo haya tangu kuanzishwa kwa programu hii mwaka 2016 na imeshapata jumla ya wahitimu 26, na tunaamini kuwa wahitimu hawa wa leo wanakuja kuleta mabadiliko makubwa katika uongozi kwenye Benki yetu”.

Alitumia pia nafasi hii, kuwasihi waajiri wote nchini kufanya mikakati ya makusudi kuruhusu viongozi wa kike kujiunga na programu hii na zingine zifananazo nahii, ili kuwajengea uwezo wa kukua na kuingia katika ngazi za juu za uongozi wa mashirika au taasisi zao.

Wengine waliohudhuria ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) pamoja Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na Mwenyekiti wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake Zanzibar (UWAWAZA), Mhe. Dkt. Saada Mkuya.