Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online,Dodoma
BENKI ya NMB juzi iliwakutanisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa mikoa ya Dodoma na Singida katika usiku wa Mtandao thabiti kwa ukuaji endelevu wa biashara.
NMB kupitia ‘Business Executive Network’ (BEN) na ‘Business Club’ wamejumuisha wafanyabiashara zaidi ya 700 kutoka Mkoa wa Singida na Babati (Manyara) kwa nyakati tofauti.
Katika usiku wa pamoja NMB walitoa mafunzo ya uendeshaji wa biashara na mikopo huku wakitangaza kiwango kikubwa cha mteja mmoja kuruhusiwa kukopa ni hadi Sh.bilioni 250 kutegemea na uwezo wake.
Meneja Mwandamizi wa NMB kitengo cha biashara Christopher Mgani amesema kutokana na kukua kwa mtaji ndani ya NMB, sasa wanaweza kutoa kiasi kikubwa na kwa marejesho ya muda mrefu kwa wateja wao.
Taarifa zinaeleza kuwa benki hiyo imefikia mtaji wa zaidi ya Sh.trilioni 7 huku ikiwa imeongoza kwa miaka nane mfululizo kuwa benki bora nchini.
Mgani amesema wameendelea kuboresha mikopo na mazingira ya ukopeshaji ambayo yamekuwa rafiki mkubwa kwa wafanyabiashara wa aina zote nchini huku wakisogeza karibu huduma za fedha kupitia NMB mkononi na Wakala zaidi ya elfu 9,000 nchi nzima.
Kingine amefafanua kuhusu mikopo ya kujenga, kumalizia au kununua nyumba ambayo alisema ni rafiki kwa kila mtu kulingana na kiwango cha mtaji wake na marejesho yake yanakwenda hadi miaka 15.
Mkuu wa kitengo cha biashara makao makuu Alex Mgeni amesema maboresho makubwa yamefanyika ndani ya benki na yote yakilenga kutoa unafuu kwa wateja wao kwa kuwa NMB ndiyo kimbilio la wote.
Mgeni amesema wamefungua milango ya majadiliano na wateja wao siku 30 kabla ya kufanya marejesho pindi wanapohisi wamekwama na benki inafanya ufuatiliaji ili kuwasaidia kujikwamua.
“Kipaumbele chetu ni kuona wateja hawapati misukosuko katika biashara zao hasa kwenye marejesho kwani kukwama kwao ni kukwama kwa benki na sisi watumishi jambo ambalo hatukubali,” amesema Mgeni.
Mmoja wa wateja wa NMB Neema Mandala amesema katika maisha yake ya biashara anajivunia kuwa na benki hiyo kutokana na kupatiwa miongozo na maelezo ya watumishi.
Neema ameomba benki kuendelea kupanua wigo wa kuwafikia wahitaji wengi zaidi katika mpango wa kuwaleta pamoja kwani wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu wa biashara.
Hata hivyo amesisitiza kwa wafanyabiashara na Watanzania wengine kutumia NMB kwa ajili ya kukuza uchumi wao kwa na kuongeza mitaji.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza