January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB washerehekea miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katika kusherekea maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar, wafanyakazi wa Benki ya NMB kutoka matawi ya Zanzibar wameungana na Baraza la Udhibiti la Mifumo wa utoaii Leseni (BLRC) Zanzibar kufanya usafi Kwenye viwanja vya Maisara.

Hii ikiwa ni ushiriki wao kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zilizopangwa na serikali katika kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi Zanzibar.

Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wa michuano ya kombe la Mapinduzi yatakayofanyika kesho uwanja wa Amaan.