January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB MastaBata KoteKote, Zaidi ya Sh117 milioni zatolewa kwa washindi 435

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Msimu huu wa sikukuu, Blue Santa kutoka Benki ya NMB yupo tayari kukuachia Zawadi za kujidai na mpaka sasa, ameshatoa zaidi ya Sh117 milioni kwa washindi 435 kupitia kampeni yake ya NMB MastaBata KoteKote ambayo inalenga kuhamasisha matumizi Ya Kadi na kuskani QR kufanya malipo Ya matumizi mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Meneja wa NMB, Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper wakati wa droo ya Sita ya wiki ya kampeni ya NMB MastaBata KoteKote iliyofanyika katika tawi la benki la Nelson Mandela iliyopo katika Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Alisema katika kampeni hiyo, zaidi ya Sh 300 milioni zitatolewa kwa washindi 854 ambapo kila wiki washindi 75 watapokea Sh Laki 1 na mshindi mmoja atashindia pikipiki, washindi 49 wakijinyakulia Sh1 milioni kila mwisho wa mwezi na wawili kujinyakulia pikipiki huku washindi 7 watajishindia tiketi za kusafiri kuelekea Dubai pamoja na wapendwa wao kwa siku 4, safari ambayo itagharamikiwa kila kitu na benki hiyo.

Vile vile, Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela, Roseline Makulukulu alisema washindi hao wanatokana na kutumia NMB mastercard au Lipa mkononi (QR) kufanya malipo kwa kutumia kadi hasa kwenye maeneo ya starehe, migahawa, kwenye maduka makubwa(supermarkets) na maduka ya kawaida.

Naye, mmoja wa washindi wa promosheni hiyo, Martha Minja ambaye alipata zawadi ya pikipiki aliwataka watanzania kuendelea kutumia Kadi zao za NMB mastercard au Lipa mkononi(QR) ili waweze kuingia kwenye droo za kushinda zawadi mbalimbali.

Huu

Usikubali mwaka uishe bila kupokea Zawadi kutoka kwa #MastaBataKoteKote! Endelea kufanya matumizi yako na NMB mastercard au Lipa Mkononi (QR) ujiweke kwenye nafasi ya kushinda zawadi ikiwemo; mkwanja, pikipiki au trip ya Dubai!