June 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB: Mafanikio ya Yanga ni matokeo ya R4 za Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline, Dar

BENKI ya NMB imedhamini uzinduzi wa Kitabu cha Historia
ya Klabu ya Yanga SC, huku Afisa Mtendaji Mkuu wa benki
hiyo, Ruth Zaipuna akisema mafanikio ya timu hiyo ni matokeo ya Falsafa ya R4 ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Falsafa ya R4 au 4R imeasisiwa kutumiwa na Rais Samia kama dira ya utekelezaji wa majukumu yake katika kuyafikia mafanikio endelevu ya taifa, hivyo Zaipuna anaamini uongozi wa Yanga umezichakata 4R hizo na kupata mafanikio ya kuigwa mfano ndani
na nje ya uwanja.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na Naibu
Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko, aliyemwakilisha Rais Samia, Zaipuna aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa mchango na mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali, ikiwemo michezo ambako Taifa limefanya vizuri.

Nadhani katika kipindi hiki, kama taifa tumeshuhudia mafanikio makubwa katika soka, ambako Taifa Stars ilifuzu tena Fainali za Afrika (AFCON 2023), na kuwa moja ya timu chache kutoka Ukanda wa CECAFA, ngazi ya vilabu nako, tumeshuhudia klabu zetu zikijenga heshima kubwa.

Unapozungumzia Falsafa ile ya 4R ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ile Reconciliation yaani Maridhiano, Resilience, Ustahimilivu au Utulivu, Reforms yaani Mageuzi au Mabadiliko na Rebuilding – Kujenga Upya, nadhani Yanga ni mfano bora wa namna ya kuzitumia hizi 4R.

“Matumizi ya falsafa hiyo yamefanikiwa kuijenga Yanga
kuwa klabu bora, imara ndani nje ya nchi, klabu inayoongozwa kwa misingi ya Utawala Bora na umoja baina ya wanachama, mashabiki, uongozi na wadau wa soka nchini Tanzania” alisema Zaipuna na kuongeza.

Yanga hii ya leo, imepitia Maridhiano yaliyoleta umoja huu tunaouona, lakini pia Yanga hii imepitia nyakati ngumu zilizohitaji Ustahimilivu wa changamoto mbalimbali, wakitambua kuwa ni sehemu ya maisha ya binadamu au taasisi tunazoziongoza.

Pia Yanga hii imepitia mabadiliko ya kiuongozi kiutawala,
kiuendeshaji na hata kiuwekezaji kwa ustawi wa klabu hii, ambayo imejijenga Upya na inaendelea kujijennga kuwa taasisi ya michezo ya kuigwa Tanzania na Afrika Mashariki, ikivutia nyota wakubwa Afrika.

“Kwa muktadha huo, nitumie nafasi hii kumpongeza kila mmoja ndani ya Yanga kwa maafanikio iliyoyapata miaka hii, ambayo yanaliletea taifa heshima” alisisitiza Zaipuna mbele ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.

Zaipuna aliishukuru Yanga kwa kuendelea kushirikiana na
NMB katika nyanja mbalimbali, na kwamba udhamini wao katika uzinduzi huo wa kitabu cha historia yao sio mwanzo wa mashirikiano baina ya pande hizo mbili zenye rekodi kubwa za mafanikio kama taasisi.

Ushirikiano wa NMB na Yanga umeanza muda sasa,
mttakumbuka mwaka jana tuliianzisha ushirikiano huu
kwa kusaini makubaliano ya mchakato wa kurahisisha usajili wa wanachama na mashabiki wa klabu hii kongwe kwa kutumia mtandao wa ma tawi yetu kote nchini