January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, wateja kuzoa Mil. 180/-

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Msimu wa Tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa kuweka pesa Benki ya NMB ‘NMB Bonge la Mpango – Moto ni Ule Ule’, umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza- Paulo Chacha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima, ambako zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 180 – zikiwemo pesa taslimu, bodaboda, pikipiki za mizigo za matairi matatu na vifaa vya nyumbani vya kieleltroniki, zitatolewa katika kipindi cha miezi mitatu.

Bonge la Mpango inalenga sio tu kuhamasisha uwekaji akiba, bali pia kurejesha kwa jamii sehemu ya faida yake, huku pia ukiwa ni mkakati wa NMB kuendelea kuwa chaguo la kwanza la wateja kwa usalama wa fedha zao pamoja na uhakika wa huduma bora na rafiki za kibenki nchini.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa NMB Bonge la Mpango katika soko la Buhongwa, madereva 10 wa bodaboda, bajaji na matoroli wanaoendesha shughuli katika soko hilo, walifunguliwa akaunti na Mkuu wa Wilaya Chacha pamoja na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi na kuwakewa kiasi cha Sh. 100,000 kwa kila mmoja ili kukidhi kigezo kikuu cha kuingia kwenye droo ya promosheni hiyo na kushinda zawadi.

Akizungumza Mponzi alibainisha kuwa, katika kipindi cha kampeni hii washindi 90 watajishindia pesa taslimu Sh. 100,000 kila mmoja (washindi 10 kila wiki NMB itakabidhi bodaboda moja kwa wiki (washindi 9 ) yenye thamani ya Sh. Mil. 2.5 ambapo zote 9 zitakuwa na thamani ya Sh. Mil. 22.7
Zawadi nyingine ni kwa wateja 10 wa droo za kila mwezi ambao watashinda bodaboda zenye thamani ya Sh. Mil. 25, huku wateja wengine 10 wa kila mwezi wakitarajiwa kujishindia pesa taslimu Sh. Mil. 1 kila mmoja.

Katika ‘Grand Finale,’ NMB itatoa pikipiki tano za miguu mitatu ‘Toyo’, thamani ya kila moja ni zaidi ya Sh. Mil. 5.5 (zote Sh. Mil. 25.55), lakini pia washindi watano watajinyakulia friji la milango miwili, TV, ‘smartphone,’ ‘washing machine’ na kompyuta mpakato ‘laptop,’ vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 14.1.

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paul Chacha pamoja na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi wakipeperusha bendera kama ishara ya kuzindua rasmi kampeni ya Bonge la Mpango – Moto Uleule, katika uzinduzi uluifanyika katika soko soko la Buhongwa jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa Benki ya NMB, Wogofya Mfalamagoha, wapili kulia ni Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi, Aikansia Muro na kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa – Ladislaus Baraka.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi (wapili kushoto) akimfungulia akaunti ya NMB dereva bodaboda katika soko la Buhongwa jijini Mwanza wakati wa kuzindua rasmi kampeni ya Bonge la Mpango – Moto Uleule. Akishuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi – Mhe. Paul Chacha (pili kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi – Paul Chacha akimkabidhi kadi ya benki dereva bodaboda katika soko la Buhongwa jijini Mwanza, baada ya kumfungulia akaunti ya NMB wakati wa uzinduzi rasmi wa Bonge la Mpango – Moto Uleule. Wakishuhudia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa – Ladislaus Baraka (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi – Aikansia Muro.