January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NLD,yatambulisha sera zake kwa wananchi

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online

VIONGOZI wa chama cha NLD,watambulisha sera za chama chao kwa wananchi, kupitia  mikutano maalumu inayofanyika  Visiwani Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu  wa NLD,Tanzania Bara,Khamis Said Hamad, akizungumza Septemba 11,2024,na viongozi mbalimbali katika ziara ya ujenzi wa chama  hicho Visiwani Zanzibar, Ameeleza kuwa ni muhimu viongozi  wa chama hicho,kujipanga kuhakikisha kinawakomboa  Watanzania.

“NLD tuna sera, zinazojibu changamoto za kijamii, kiuchumi na  kisiasa.Viongozi enezeni sera hizo ili  kuwavutia wananchi zaidi,”.

 Pia ametoa wito kwa viongozi hao,kuandaa wagombea wenye sifa, waaminifu, wenye nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi, kwenye ngazi za mitaa na vijiji, pamoja na uchaguzi mkuu.

Ziara ya chama hicho ni ya siku nne, ambapo itakuwa ikiongozwa na Katibu Mkuu   Doyo Hassan Doyo, ambapo inaendelea  Leo Septemba 12, 2024 Visiwani Zanzibar.