Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
WANACHAMA 150 kutoka ADC na ACT wamejiunga na NLD na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. Doyo Hassan Doyo. Wanachama hao, wakiongozwa na Mariam Sijaona aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ACT Wazalendo na Scola Kahana aliyekuwa mgombea wa nafasi ya makamo mwenyekiti bara kupitia ADC na mgombea ubunge jimbo la kibaha katika uchaguzi wa 2020, tarehe 29-09-2024 wamejiunga na Chama cha NLD.
Mhe. Doyo, pamoja na viongozi wengine wa NLD, akiwemo Makamo Mwenyekiti Bara, Mhe. Khamis Said Hamad, waliwakaribisha wanachama hao wapya na kuwahakikishia kuwa wana haki sawa na wanachama wa chama hicho kwa mujibu wa katiba ya NLD.
Wanachama hao wamesema kuwa wameamua kujiunga na Chama cha NLD kwa sababu ni haki yao ya kikatiba na kuunga mkono juhudi za Mhe. Doyo katika kukuza demokrasia nchini.
“Tunajua chama chetu kipya hakina ruzuku, lakini tupo tayari kukaa na njaa ili kupigania demokrasia ya kweli na hatimaye chama chetu kufanya vizuri kwenye chaguzi zijazo,” walisisitiza wana chama hao.
Mhe. Doyo aliwasihi wanachama hao wapya kusoma Itikadi ya NLD, akisisitiza kuwa Itikadi ya chama hicho imebeba uzalendo, haki, na maendeleo.
Chama cha NLD kinatarajia kufanya ziara Pemba, Tanga, na maeneo mengine nchini.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best