January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nje Sports yaigalagaza timu ya Ikulu Zanzibar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) imeigalagaza timu ya mpira wa miguu kutoka Ofis ya Rais Ikulu Zanzibar magoli 8 – 3 katika mchezo ulichezwa uwanja wa Mao zedong’s Unguja, Zanzibar.

Nje Sports iliutawala mpira kwa asilimia kubwa ambapo kipindi cha kwanza iliongoza kwa magoli 5 – 1. Magoli ya nje sports yalifungwa na Ramadhani Chambuso (1), Said Kasanga (2), Selemani Mkonde (2), Fabian David (1) pamoja na Yakubu Kibiga (1).

Magoli ya timu kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar yalifungwa na Khamis Ramadhan (1) pamoja na Seif Hatibu Ally (2).

Ushindi wa Nje Sports umeiwezesha kusonga mbele ambapo tarehe 11 Januari 2024 itacheza na Hazina katika uwanja wa Mao zedong’s Unguja, Zanzibar majira ya saa 16:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa timu ya Nje Sports, Shaban Maganga amesema kuwa lengo la timu yake ni kuimarisha kikosi na kujihakikishia ushindi katika michezo inayaofuata. Kadhalika kocha huyo ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuwawezesha vyema hadi kufikia hatua hiyo.