May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIT kutosa Milioni 120.4 mafunzo ya urubani

Na Mwandishi Wetu, timesmajira

MKUU wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa amesema chuo hicho kitatoza Dola za Marekani 48,000 sawa na Sh. Milioni 120.4 kwa mafunzo ya urubani ambayo ni sawa na nusu ya gharama ya nje ya nchi ya Dola 100,000 sawa na Sh. Milioni 200 hadi 300.

Aidha, ameishukuru serikali kwa ndege mbili walizokabidhiwa na kusesema kuwa chuo kipo katika hatua za mwisho za kuanza kutoa mafunzo ya urubani kwa gharama nafuu ya asilimia 50 ulilinganisha na vyuo vya nje.

Profesa Mganilwa ameyasema jijini Dar es Salaam na Profesa Zacharia Mganilwa wakati wa uzinduzi wa ndege mbili aina ya Cessna Skyhawk za mafunzo ya Urubani kwa chuo hicho cha NIT.

“Mafunzo ya urubani yanaonekana kuwa ni taaluma ya watoto wa matajiri tu, lakini je Tanzania kuna matajiri wangapi, ila pia serikali kutoendelea kutoa ufadhili wa mafunzo ya urabani na uhandisi kwa muda mrefu imekuwa pia ikipunguza wanafunzi kusomea fani hii,”, amesema Profesa Mganilwa.

Amesema, kumekuwepo na uhaba wa wataalamu wa sekta ya anga wakiwemo marubani jambo linalopelekea serikali kuajiri wataalamu kutoka nje ya nchi.

Profesa Mganilwa amesema takwimu zilizopo zinaonesha kuwa, wenye leseni ya biashara katika eneo la usafiri wa anga waliosajiliwa ni 551 ambapo kati yao wageni ni 352 sawa na asilimia 64 na wazawa ni asilimia 36.

“Wakufunzi na marubani wanafunzi wameaswa kuzitunza ndege hizo ili ziweze kudumu na kuendelea kufundishia marubani walio wengi zaidi,” amesema