March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIDA kuweka kambi Tabata kuanzia leo

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online-Dar- es-Salaam

MAMLAKA ya Vitamburisho vya Taifa ( NIDA )inatarajia kuweka kambi maalum kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakazi wa Jimbo la Segerea katika ofisi ya Kata ya Tataba kuanza leo Januari 5 hadi Januari 14,2026.

Mratibu wa kampeni hiyo awamu ya kwanza Heri Shabaan,amesema kwa kushirikiana na ofisi ya Serikali ya Mtaa Mtambani, anaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuanzia miaka 18 na kuendelea ili kuweza kujiandikisha na kupata vitambulisho vya NIDA.

Heri amesisitiza wananchi kufika na viambatanisho vyote muhimu vinavyohitajika ili kurahisisha zoezi hilo kwani watakuwepo Maofisa wa NIDA pamoja na wa Idara ya Uhamiaji .

Amewaomba Wenyeviti wa Serikali za mitaa katika Jimbo la Segerea kwa kushirikiana na Maofisa Watendaji kuwatangazia wananchi wao ili waweze kupata fursa hiyo karibu na makazi yao