January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIC yazindua msimu wa pili kampeni ya NIC KITAA

Na Penina Malundo, Timesmajira

KATIKA kuendeleza sera ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya bima kwa wote
Shirika la Taifa la Bima (NIC) limezindua msimu wa pili wa Kampeni ya ‘NIC KITAA’ yenye lengo la kutoa elimu ya Bima kwa watanzania ili waweze kutambua faida na muhimu wake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Kaimu Mkeyenge amesema kampeni hiyo itafanyika mtaa Kwa mtaa ili kuhakikisha elimu ya bima inamfikia kila mtanzania.

“Tunaingia msimu wa pili wa kampeni ya NIC Kitaa lengo ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wote na kutambua umuhimu wa bima”amesema

Mkenyenge amesema pamoja na kutoa elimu kampeni hiyo itatoa fursa k watanzania pia tatambatisha na kuandikisha bima kwa wateja wapya.

Amesema na kwa upande wa wale wanaolipa madeni sio lazima waende ofisini na badala yake wamesogezewa huduma mtaani.

Aidha amesema kampeni hiyo itafanyika nchi nzima na kwa sasa wameanza na mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Singida.