November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIC yaja na mikopo midogo ya NISOGEZE

Na Penina Malundo,Timesmajira

SHIRIKA la Taifa la Bima(NIC)imeanzisha huduma ya mikopo midogo  midogo ya muda mfupi kwa wateja wake wenye Bima ya Maisha ijulikanayo kwa jina la NISOGEZE kwa lengo la kutatua changamoto za muda mfupi zinazowakabili wateja wa bima hiyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ”Sabasaba”,Afisa Bima Upendo Shengena amesema Shirika hilo kwa kushirikia na Benki ya TCB,ilianzisha huduma hiyo ili kusaidia wateja wa bima za maisha kwa NIC.

Amesema huduma hiyo inafaida mbalimbali ikiwemo kumuwezesha mteja wa Bima ya Maisha kupata mkopo kwa haraka kwa kutumia simu ya kiganjani na kupata mkopoa wenye riba nafuu.

‘Bima ya Maisha ni mkataba baina ya mteja na Kampuni ya Bima ambapo mteja analipa ada ya bima kidogo kidogo kwa lengo la kupata fidia au mafao endapo atapatwa na janga au kumaliza muda wa mkataba,”amesema na kuongeza

”Kigezo cha kupata mkopo wa Nisogeze ni kuwa na hati ya Bima ya Maisha kutoka katika Bima ya NIC ambapo mteja aliyechangia ada ya bima kuanzia mwezimmoja anaweza kunufaika na huduma hiyo ya mkopo,”amesema

.Aidha Shengena  amesema huduma hiyo inatoa jawabu la haraka kwa shida ya kifedha kwa wateja wa Bima za Maisha kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu kwa kutumia simu ya kiganjani.

Amesema pia ni mkopo ambao unawaondolea wateja wa Bima hiyo ya Maisha usumbufu na gharama zinazotokana na mikopo.