December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIC washirikiana na wadau kuanzisha uandaaji wa sera ya kilimo na mifugo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Shirika la Bima na Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwemo Mfuko wa kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) wamepanga kuanzisha uandaaji wa sera ya Kilimo na mifugo ambayo itaelezea kwa kias kikubwa namna ambavyo wanaweza kutekeleza Bima ya Kilimo na Biima kwaajili ya mifugo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kutembelewa na Kamishna wa Bima Nchini Dkt. Baghayo Saqware, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Elirehema Doriye amesema ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija na kilimo ambacho kinavutia watanzania wengi mojawapo ya vitu vya msingi ni kuhakikisha bima ya kilimo inakuwepo lakini pia sera za kilimo zinaenda kugusa wakulima wadogowadogo na kuhakikisha kwa umoja wao wanaweza wakazalisha.

“Bima ya kilimo kazi yake kubwa ni kuhakikisha inamuondolea hasara ambazo mkulima anawezapata kutokana na majanga mbalimbali kama mvua iliyozidi, wadudu ambao wanashambulia mazao , mvua za mawe, ukame na vitu vyote ambavyo vinaweza kuathiri kilimo na uzalishaji”. Amesema

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mfuko wa kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Jackline Machango amesema wameona umuhimu katika suala hilo hivyo wameamua kuweka mkono wao kuona ni namna gani wanaweza kusaidiana na TIRA pamoja na NIC kuandaa Sera hiyo ya Bima pamoja na kuitekeleza kwa kiwango ambacho kinaweza kuonekana kwa kiasi gani sera hii inaweza kufanya kazi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kuzindua ofisi mpya ya Shirika la Bima la Taifa (NIC), Kamishna wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware ameiopongeza NIC kwa kazi ambazo wanazifanya hasa kuhakikisha wanamjali mteja kuanzia utoaji huduma pamoja na eneo la utoaji huduma.

Aidha amewataka watumishi wa NIC kuhakikisha wanaendelea kuongeza juhudi katika kazi pia kuhakikisha ofisi zote za shirika hilo zinakuwa vizuri na salama kwaajili ya utoaji huduma kwa Watanzania.