Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Shirika la Bima la Taifa ( NIC) limeendelea kuimarika kibiashara ambapo kuanzia mwaka 2012 hadi 2021 ni mwaka mmoja ndiyo ambao walienda chini zaidi ya miaka mingine iliyopita lakini pia kwa miaka mitatu iliyopita wamekuwa na muendelezo katika upatikanaji wa faida ambayo ndiyo msingi wa kuhakikisha shirika linaishi kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa (NIC) Dkt. Elirehema Doriye katika katika kikao kazi na wafanyakazi wa Shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mwaka huu 2021 umekuwa na matokeo mazuri lakini pia umekuwa wenye nguvu ambazo zinahitaji wao kama NIC kubadirika na kuendelea kukabiliana na changamoto;
“Mwaka huu 2021 nao umekuwa mzuri ambao umekuwa na matokeo mzuri lakini pia wenye nguvu nyingi ambazo zinahitaji pia sisi kubadirika na tuendelee kukabiliana kwenye changamoto mpya kwasababu kila mwaka na kila wakati changamoto mpya zinakuja”
Aidha Dkt. Elirehema amesema Bila NIC soko la Bima Tanzania haliwezi kuendelea , kwahiyo lazima wajue nafasi yao na waoneshe uwezo wao katika kuwahudumia watanzania.
Dkt. Doriye amewasihi wafanyakazi wa Shirika hilo katika Kuelekea mwisho wa mwaka kuendelea kuwa imara kwa kufanya kazi kwa bidii ili ibaki kuwa historia;
“Tunapofunga mwaka 2021 tukumbuke kwamba yote ambayo yamefanyika 2021 yanakuwa historia, tunafungua ukurasa mwingine mpya wa 2022 ambayo inahitaji ufikiriaji mpya, utendaji mpya, ufanyaji kazi uliotukuka ili kuendeleza mafanikio tuliyopata miaka iliyopita au mwaka huu”
“Tunatakiwa tuwe wabunifu, tufikirie zaidi, tufanye kazi zaidi, tuwe hatari kwenye utafutaji wa Masoko na wateja wetu wafurahi kuliko mwaka uliopita na katika kila shughuli zetu tunazozifanya hakikisha mteja yupo katikati ya vitu tunavyovifanya” alisema Dkt. Doriye
Mbali na hayo Dkt. Doriye amesema kuwa NIC wamekuwa sehemu ya mabadiliko na kuyafanyia kazi mabadiliko hayo;
“Nashukuru kwa sehemu kubwa tumekuwa sehemu ya mabadiliko pia tumekuwa sehemu ya kuyakubali na kuyafanyia kazi mabadiliko hayo kwasababu mabadiliko yoyote ambayo yanania njema yatatufikisha sehemu ambayo tunastahili kuwepo” alisema Dkt. Doriye
Mkurugenzi huyo alimaliza kwa kuwashukuru wafanyakazi wa (NIC) kwa kwenda pamoja, mbali na changamoto nyingi walizokutana nazo lakini wameshikamana na kuendelea kupata mafanikio.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba