January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ni Ndugai tena

Na Angela Mazula, TimesMajira Online

WABUNGE wamemchagua mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai kuongoza kiti cha uspika kwa kumpa kura ya ndio huku kura mmoja ikimkataa.

Ndugai alikuwa mgombea pekee wa kiti hicho uliofanyika Dodoma leo.

Akitangaza ushindi huo mwenyekiti wa muda Mbunge wa Jimbo la Ismani William Lukuvi amesema kuwa ushindi alioupata ni sawa na asilimia 99.7.

Spika Ndugai ameapa mbele ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuitumikia vyema Jamuhuri na kutenda haki kwa watu wote kwa mujibu wa  katiba, kanunu za bunge na sheria.