Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limezishukuru Taasisi, Idara na Wizara zilizotimiza wajibu wao kwa kulipa kodi ya pango na malimbikizo wanayodaiwa.
Taasisi hizo zimelipa kodi na malimbikizo wanayodaiwa baada ya agizo la Serikali la kuzitaka taasisi zote za umma, Wizara, Idara za Serikali na wakala za Serikali zinazodaiwa malimbikizo ya kodi ya pango na NHC ziwe zimeshalipa madeni yao kabla Mei 30, 2020 (kesho).
Taarifa imetolewa kwa vyombo vya habari na NHC Makao Makuu jijini Dar es Salaam jana ilipongeza taasisi zilizoitikia wito huo, kwa kulipa kodi ya pango na malimbikizo wanayodaiwa.
Hata hivyo, taarifa hiyo imeeleza kwamba zipo taasisi kadhaa ambazo hazijatimiza wajibu wao wa kulipa kodi na malimbikizo yao wanayodaiwa na Shirika.
“Tunapenda kuzihimiza taasisi ambazo hazijatekeleza agizo la Serikali zijitahidi kulipa madeni yao kabla Shirika halijawasilisha taarifa rasmi ya ulipaji wa madeni kwa Mamlaka kwa hatua stahili,” imefafanua taarifa hiyo.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi