Na Rose Itono, timesmajira
MBUNGE wa VIti Maalum Mkoa wa Dar es salaam Janeth Masaburi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Taasisi zingine za Ujenzi kuhakikisha zinaendeleza ujenzi na ubunifu kwenye miradi yao ya ujenzi Ili kuwa na makazi bora
Akizungumza kwenye ziara iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake (UWT ) Kinondoni kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
Ukiwepo wa Samia Housing Skill Kawe Manispaa ya Kinondoni
Masaburi amesema ili kuwa na makazi bora ni lazima NHC na Taasisi Nyingine za Ujenzi zikaangalia namna ya kuboresha makazi kwenye Jiji la Dar es Salaam
Amesema ili Shirika liendane na taswira ya mkoa linapaswa kujenga nyumba zenye ubora na kwa gharama nafuu
“Ujenzi wa nyumba za gharama nafuu utawezesha kila mwananchi mwenye kipato cha chini kuweza kumiliki nyumba zenye hadhi ya maghorofa,” amesema Masaburi.
Ameongeza kuwa wananchi wanahamu sana ya kutaka kuishi kwenye nyumba hizo ila wanashindwa kwa sababu ya gharama kubwa
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC Meneja wa Habari na Uhusiano Muungano Saguya amesema mradi huo umetengeneza ajira kwa watanzania zaidi ya 700 na kugharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 48.27 ambapo hadi sasa Bilioni 14 zimeshatumika .
Amesema mradi huowa nyumba 560 za makazi kwenye maghorofa kumi
ulianza Novemba 2022 na unatarajia kukamilika Aprili 2024.
“Mradi huu unatarajia kuleta faida kubwa kwa wakazi wa Dar es salaam, na kwamba pamoja na kujenga nyumba za gharama hizi pia awamu ijayo itajenga nyumba za gharama nafuu ili kila mwananchi aweze kumudu gharama hizo na kunufaika na miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Naye Mhandisi wa mradi huo, Grace Musita amamshukuru Rais na Serikali kwa kuwaamini wahandisi wanawake kwa kupewa miradi mikubwa na kuisimamia ipasavyo, na huku akiahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha ujenzi unapokamilika kila mtu anaishi kwenye mazingira bora.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam