January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NHC kuzindua sera ya ubia tarehe 14 Novemba,2022

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline, Dodoma.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa kuwa mgeni rasmi siku ya uzinduzi wa  sera ya ubia ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC),inayolenga masuala ya uwekezaji ambapo kwa kipindi cha miaka mitano inategemewa kuwa na miradi 200 ya ubia yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 400.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara  ya Nyumba ya Taifa, William Genya ambapo uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba, 14 mwaka 2022.

Genya amesema kuwa sera hiyo ilianza kufanya kazi tangu mwaka 1993 na hapo katikati iliweza kufanyiwa maboresho mara nne na hayo yote yamekuwa yakilenga kuweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji lakini pia kuipa shirika hisa zaidi katika miradi.

Amesema kuwa wameboresha sera hiyo kwa kuweka vitu vinne ambavyo mwekezaji yeyote anaweza akaangalia ambavyo vinaweza vikamfaa na kuomba kufanya nao kazi.

“Vitu hivyo ni pamoja na kutumia ardhi yetu kama mtaji ambapo tumeweka bidhaa mbili  moja inampa mbia umiliki wa asilimia 40 mwishoni mwa miaka 15 ya uwekezaji, pia inampa mbia asilimia 25  baada ya mika 25 ya uwekezaji kwenye mradi”amesema Mngenya.

Pia shirika kuweka ardhi na fedha kama mtaji na  mbia anaweka fedha halafu tunatekeleza mradi kwa pamoja ,nahii ni kwa ile miradi mikubwa ambayo thamani yake  inazidi bil.50 na zaidi.

Kitu kingine ni Kujenga,kuuza na kugawana ambapo shirika linaweka ardhi na mbia anaweka fedha ambapo jengo  linajengwa halafu linauzwa lote na shirika na  mbia wanagawana mapato yaliyotokana nakuuza  jengo hilo  kutokana na umiliki wa hisa kwenye mradi.

Pamoja na Shirika kutoa ardhi kwa mkataba wa miaka 10 hadi 30 ,halafu mbia anajenga na kuendesha jengo lile na baada ya muda wa mkataba kuisha anarudisha jengo lile kwa NHC”amesema.

Alisema kuwa tangu kuanza kwa utaratibu huo jumla ya miradi 111 ilitekelezwa ikiwa na thamani ya bil.300,ambapo katika miradi hiyo miradi 81 yenye thamani ya sh.bil 240 imekamilika na kuanza kutumika huku miradi 30 yenye thamani ya bil.60 inaendelea kukamilishwa.

“Miradi hii imechangia upatikanaji wa ajira, kuboresha mandhari ya miji yetu,kuongeza mapato ya shirika,kuongeza wigo wa kodi za serikali, kuongeza maeneo kwaajili ya biashara na makazi na kuipanga miji yetu,

“Sasa thamani ile ya bil.300 ile thamani ya  hisa za shirika kwenye miradi ambapo hisa hizo katika miradi hiyo kuna za asilimia 25 kwenye baadhi ya miradi mpaka asilimia 50, hivyo dhamani ya miradi yote kwa ujumla zikiwemo hiza za wabia ni zaidi ya Tril. 1.2,”amesema.

Kwa upande wake Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya amesema kuwa washiriki 1000 kutoka taasisi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na binafsi ,vyama na bodi za kitaaluma pamoja na wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi.

Saguya amesema  kuwa uzinduzi wa sera ya ubia unaenda kufungua milango ya uwekezaji  kwenye sekta ya nyumba na kwa hakika wanaunga mkono maono na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuvutia uwekezaji nchini kwa kuruhusu sekta binafsi ambayo ni injini ya kuleta maendeleo ili iwekeze mitaji yao kujenga uchumi wa Taifa .

“Sera ya ubia ambayo tunawaalika wawekezaji kushiriki ilianzishwa na shirika tangu mwaka 1993 na kufanyiwa maboresho kadhaa kulingana na wakati husika”amesema.

Aidha amesema kuwa maboresho ya mwisho yalifanyika mwaka 2022 na yamezingatia kuvutia uwekezaji kwa kuwa yana maslahi kwa shirika na mwekezaji.

“Lakini pia Mabalozi wa nchi  zenye wawekezaji wakubwa wamealikwa na wawakilishi wa kamati za Bunge zinazogusa shughuli za shirika”amesema.