May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NFRA inavyodhibiti mfumko wa bei ya mazao

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

AFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula Nchini (NFRA)  Milton Lupa amesema moja ya majukumu yanayofanywa na Wakala huo ni pamoja na kunua na kuhifadhi chakula, kutoa chakula wakati wa dharula ama wakati wa majanga yanayojitokeza ndaniya nchi na jukumu la tatu ni kuuza chakula ambacho muda wake wa kuhifadhi umekwisha ili kuweza kununua akiba mpya.

Akizungimza na waandishi wa habari katika maonyesho ya wakulima Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya,Lupa amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kunakuwepo na usalama wa chakula nchini.

Aidha Lupa amesema,jukumu lingine walilopewa siku za hivi karibuni ni kudhibiti mfumuko wa bei pale mahindi yanapopanda bei.

“Pamoja na majukumu mengine siku za hivi karibuni tumepewa  ambapo pale mahindi yanapokuwa bei ya juu wao wanatoa mahindi kwa bei ya chini ili kusababisha wafanyabiashara wapunguze kwa bei.

Kuhusu maonyesho ya wakulima amesema,wapo katika maonyesho hayo kwa ajili ya kuonyesha wakulima jinsi ya uhifadhi wa mazao .

Aidha amesema, nafaka ambazo kwa sasa wananunua na kuhifadhi ni mahindi, mpunga pamoja na mtama na kuongeza kuwa kwa sasa wamefungua vituo katika kanda zote.

“Tunachokifanya tunanunua kwa bei ambayo ipo juu ya soko ili kuwawezesha wakulima kupata pesa zitakazowawesha  wawezesha  kurudui mashambani kuendelea kufanya uzallishaji wa mazao kwa misimu inayofuata.”amesema Lupa Amesema mpaka sasa tayari wameshanunua tani zaidi ya 75,000 za mazao huku akisema matarajio yao ni kununua zaidi ya tani 300,000.

Ametumia nafsi hiyo kuwasihi wakulima kupeleka mahindi NFRA ili yanunuliwe kwa bei nzuri lakini pia wajiwekee akiba kwani likitokea janga lolote la njaa NFRA hurudisha chakula hicho kwa wananchi.