Na Joyce Kasiki,Dodoma
WAKALA wa Uhifadhi wa Chakula Nchini (NFRA) ,umeanza kutumia mfumo wa kidijitali katika kupima mahindi ili kuleta tija kwa mkulima.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dkt.Andrew Komba ameyasema hayo katika maonesho ya wakulima na wafugaji (88) viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yaliyoanza Agosti Mosi na kufikia kilele chake Agosti 8 mwaka huu.
Amesema mfumo huo ambao ni mizani ya kidijitali hiyo inaonesha namna ambavyo mkulima atapata faida na uhakika wa mazao anayouza NFRA.
“Wakulima wameipokea mizani hii vizuri wakiamini kwamba inawawezesha kupata kiwango sahihi wanachotuuzia na sisi kwetu inatupa record ‘ kumbukumbu’ sahihi kwa sababu inaingiza taarifa katika mfumo ambao unatumika katika suala zima la kuhifadhi .”amesema Dkt.Komba
Aidha amesema ,Wakala huo una jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa na usalama wa chakula
Kwa mujibu wa Dkt.Komba,ili kulitekeleza jukumu hilo NFRA wamekuwa wakinunua na kukusanya chakula na kuhifadhi vizuri kwa utaratibu wa kuhakikisha afya na usalama wa mlaji.
“Kwa ili kuhakikisha chakula kinakuwa salama wakati wote ,tunatumia maghala na vihenge katika kuhifadhi chakula,lakini pia tunawafundisha wakulima kuhifadhi chakula wanacholima katika hali ya usalama badala ya kuhifadhi kizamani.”amesema Dkt.Komba
Amwsema chakula wanachohifadhi kinalenga kuisaidia jamii pale panapotokea uhaba wa chakula na kuwafanya wawe na uhakika wa chakula.
More Stories
Prof.Muhongo kufanya mkutano wa dharura kujadili ufunguzi Sekondari ya Nyasaungu
Bilioni 8.6, kutumika kwa ruzuku nishati safi ya kupikia
Waipongeza Serikali miradi ya zaidi ya tirioni moja